Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 126. Eneo la Vikao vya Bunge

(1) Vikao vya Bunge lolote vinaweza kufanyiwa sehemu yoyote nchini Kenya, na kuanza wakati wowote utakaoteuliwa na Bunge.

(2) Kila kutakapochaguliwa Bunge jipya, Rais, kwa kupitia notisi ya Rasmi la Serikali, atateua mahali na tarehe ya kikao cha kwanza cha Bunge jipya, ambayo haitakuwa zaidi ya siku thelathini baada ya uchaguzi.