Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 125. Uwezo wa Kuitisha Ushahidi

(1) Bunge lolote na kamati yoyote yake, lina uwezo wa kumuita mtu yeyote kwa kusudi la kutoa ushahidi mbele yake.

(2) Kwa lengo la ibara ya (1), Bunge na kamati yake nyingineyo ina uwezo sawa na Mahakama Kuu–

  • (a) kuhakikisha kuhudhuria kwa mashahidi na kuwahoji chini ya kiapo, kuthibitisha au vinginevyo;
  • (b) kushurutisha utoaji wa nyaraka; na
  • (c) kutoa agizo au ombi la kuwahoji mashahidi walio katika mataifa ya nje.