Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 113. Kamati za Upatanishi

(1) Iwapo Mswada utapelekwa kwa kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 112, Maspika wa Mabunge yote mawili watateua kamati ya upatanishi itakayohusisha idadi sawa ya wanachama wa Mabunge yote mawili ili kujaribu kutengeneza toleo jingine la Mswada litakalokubalika na Mabunge yote mawili.

(2) Iwapo kamati ya upatanishi itakubaliana na toleo hilo la Mswada, basi kila Bunge litapiga kura ili kupitisha au kukataa toleo hilo la Mswada.

(3) Iwapo Mabunge yote mawili yanakubali ttole hilo la Mswada kama ilivyopendekezwa na kamati ya upatanishi, Spika wa Baraza la Kitaifa atamkabidhi Rais ili kuidhinishwa.

(4) Iwapo kamati ya upatanishi itakosa kuafikiana kuhusu toleo hilo la Mswada kwa kipindi cha muda wa siku thelathini, au iwapo toleo hilo lililopendekezwa na kamati litakataliwa na na mojawapo ya Mabunge, basi Mswada huo utakuwa umeshindwa.