Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 86. Upigaji Kura

Katika kila uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itahakikisha kwamba–

  • (a) katika njia yoyote ya upigaji kura itakayotumiwa, mfumo unakuwa rahisi, sahihi, wa kuthibitika, salama, unaowajibika na ulio na uwazi;
  • (b) kura zinazopigwa zinahesabiwa, kuorodheshwa na matokeo kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura hapo kituoni;
  • (c) matokeo kutoka kwa vituo vingine vya upigaji kura yanajumlishwa kwa uwazi na kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura; na
  • (d) miundo na taratibu mwafaka zimewekwa ili kuondoa uwezekano wa kuhusishwa kwa mienendo yoyote mibaya, ukiwemo uhifadhi salama wa vifaa vya uchaguzi.