Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 82. Sheria Kuhusu Uchaguzi

(1) Bunge litatunga sheria ya kutoa nafasi ya–

 • (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuamua idadi ya maeneo-bunge kuhusu maeneo ya uchaguzi kwa wanachama wa Baraza la Kitaifa na mabaraza ya kaunti;
 • (b) uteuzi wa wagombeaji;
 • (c) usajili wa mara kwa mara wa raia kama wapiga kura;
 • (d) hali ya chaguzi na kura za maamuzi. Uendeshaji na usimamizi bora wa chaguzi na kura za maamuzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombeaji wa uchaguzi; na
 • (e) usajili wa mara kwa mara wa raia wanaoishi nje ya Kenya, kama wapiga kura na kuzifahamu haki zaomza kupiga kura.

(2) Sheria inayotakikana na ibara ya (1) (d) itahakikisha kwamba upigaji kura katika kila uchaguzi ni–

 • (a) rahisi;
 • (b) wazi; na
 • (c) inazingatia mahitaji maalumu ya-
  • (i) watu wenye ulemavu; na
  • (ii) watu wengine ama vikundi vya watu walio na mahitaji maalumu.