Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 65. Umilikaji Ardhi wa Wasio Raia

(1) Mtu asiye raia anaweza kumiliki au kutumia ardhi kwa misingi ya kukodisha pekee, na mkataba huo hata ukitolewa hautazidi miaka tisini na tisa.

(2) Masikizano, makubaliano au uhawilisho wa aina yoyote unaompa mtu asiye raia wa Kenya uwezo wa kumiliki ardhi kwa zaidi ya miaka tisini na tisa utachukuliwa kwamba maafikiano hayo ni ya miaka tisini na tisa na wala sio zaidi.

(3) Kwa madhumuni ya Kifungu hiki–

  • (a) kampuni au shirika lolote litakubaliwa tu kama raia iwapo shirika hilo linamilikiwa kabisa na raia mmoja au zaidi;
  • (b) mali inayoshikiliwa kama amana itachukuliwa kama inayomilikiwa na raia iwapo tu faida ya manufaa yote ya amana hiyo inashikiliwa na raia.

(4) Bunge linaweza kutunga sheria kuweka masharti zaidi ya utekelezaji wa Kifungu hiki.