Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 55. Vijana

Serikali itachukua hatua, ikiwemo miradi ya vitendo sawazishi, kuhakikisha kwamba vijana–

  • (a) wanapata elimu na mafunzo yanayofaa;
  • (b) wana fursa ya kujumuika, kuwakilishwa na kushiriki katika nyanja za kisiasa, kijamii kiuchumi na nyanja nyingine za maisha;
  • (c) wanapata kazi; na
  • (d) kulindwa dhidi ya tamaduni zinazodhuru na kunyanyasa.