Kifungu 52. Ufafanuzi wa Sehemu Hii
Sehemu hii haitafasiriwa kama kuwekea mipaka au kustahilisha haki yoyote.
Kifungu 53. Watoto
Maslahi ya mtoto ni muhimu sana katika kila suala linalomhusu mtoto.
Kifungu 54. Watu Wenye Ulemavu
Serikali itahakikisha kwamba angalau asilimia tano ya maafisa katika mashirika ni watu wenye ulemavu.
Kifungu 55. Vijana
Serikali itachukua hatua kuhakikisha kwamba vijana wanapata elimu na mafunzo yanayofaa.
Kifungu 56. Makundi Yaliyotengwa na Kubaguliwa
Serikali itatekeleza mipango inayonuia kuhakikisha kuwa makundi yaliyotengwa na kubaguliwa yanashiriki na kuwakilishwa katika uongozi na nyanja zote za maisha.
Kifungu 57. Wazee Katika Jamii
Serikali itachukua hatua kuhakikisha haki za wazee kushiriki kikamilifu katika masuala ya jamii.