Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 47. Hatua ya Haki za Kiutawala

(1) Kila mtu ana haki ya vitendo vya utawala ambavyo ni vya haraka, fanisi, vya kisheria , vinavyofaa na sawa.

(2) Kila mtu ambaye haki yake au uhuru wake wa kimsingi umeathiriwa au unaweza kutatizwa kabisa na hatua ya kiutawala, ana haki ya kupewa sababu kwa njia ya maandishi kuhusu hatua hiyo.

(3) Bunge litatunga sheria ya kuidhinisha haki zilizotajwa katika ibara ya (1) na sheria hiyo–

  • (a) itatoa nafasi ya kurekebishwa kwa hatua hiyo ya kiutawala na mahakama au, ikiwezekana mahakama huru isiyoegemea upande wowote; na
  • (b) kuendeleza uongozi unaofaa.