Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 33. Uhuru wa Kujieleza

(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujieleza unaohusisha–

  • (a) uhuru wa kutafuta, kupokea au kutoa habari au kauli;
  • (b) uhuru wa ubunifu wa kisanii; na
  • (c) uhuru wa kiakademia na utafiti wa kisayansi.

(2) Haki ya uhuru wa kujieleza haiambatani na–

  • (a) propaganda ya vita;
  • (b) uchochezi wa ghasia;
  • (c) hotuba za chuki; au
  • (d) utetezi wa chuki ambao–
    • (i) unajumuisha uchochezi wa kikabila, kuwatusi wengine au uchochezi wa kusababisha maafa; au
    • (ii) unaotokana na misingi yoyote ya ubaguzi iliyotajwa au kuonyeshwa katika Kifungu cha 27 (4).

(3) katika kutekeleza uhuru wa kujieleza, kila mtu ataheshimu haki na hadhi ya watu wengine.