Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 254. Kuripoti kwa Tume na Afisi Huru

(1) Mwishoni mwa kila mwaka wa makadirio ya fedha, kila tume na anayeshikilia wadhifa wa afisi huru, watawasilisha ripoti kwa Rais na Bunge, haraka iwezekanavyo.

(2) Wakati wowote, Rais, Baraza la Kitaifa au Seneti wanaweza kuitaka tume au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru kuhusu suala lolote kuwasilisha ripoti kuhusu suala mahususi.

(3) Kila ripoti itakayohitajika kutoka kwa tume au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru chini ya Kifungu hiki, itachapishwa na kutangazwa.