Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 252. Majukumu na Mamlaka ya Jumla

(1) Kila tume, na anayeshikilia wadhifa wa afisi huru–

  • (a) anaweza kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi au kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mwananchi;
  • (b) ana mamlaka muhimu ya kupatanisha, kusuluhisha na kujadiliana ili kupata maafikiano;
  • (c) itaajiri wafanyakazi wake; na
  • (d) inaweza kutekeleza majukumu na mamlaka mengine yoyote iliyopewa na sheria, mbali na majukumu na mamlaka iliyopewa na Katiba hii.

(2) Malalamiko kwa Tume au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru yanaweza kuwasilishwa na mtu yeyote mwenye kibali cha kuendeleza mashtaka chini ya kifungu cha 22 (1) na (2).

(3) Tume na afisi huru zifuatazo zina mamlaka ya kumwita shahidi kutoa usaidizi kwa madhumuni ya kufanya uchunguzi wao–

  • (a) Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Usawa ya Kenya;
  • (b) Tume ya Huduma za Mahakama;
  • (c) Tume ya Kitaifa ya Ardhi;
  • (d) Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu.