Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 236. Kuwalinda Wafanyikazi wa Umma

Afisa wa umma hataweza–

  • (a) kuonewa au kubaguliwa kwa kutekeleza majukumu ya kiafisi kwa mujibu wa Katiba hii au sheria nyingine yoyote; au
  • (b) kufutwa, kuondolewa afisini au kushushwa cheo au kuadhibiwa bila kufuata utaratibu wa sheria.