Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 231. Benki Kuu ya Kenya

(1) Benki Kuu ya Kenya imeundwa.

(2) Benki Kuu ya Kenya inawajibikia kuelekeza sera za kifedha, kudumisha udhabiti wa bei, kutoa sarafu na kutekeleza majukumu mengine kama yalivyotolewa na sheria ya Bunge.

(3) Benki Kuu ya Kenya haitakuwa chini ya mamlaka au kuelekezwa na mtu au shirika lolote inapokuwa inatumia mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake.

(4) Noti na sarafu zinazotolewa na Benki Kuu ya Kenya zinaweza kuwa na picha zinazoashiria Kenya au kifungu cha Kenya lakini zisiwe na picha ya mtu yeyote.

(5) Sheria ya Bunge itatoa mwongozo, wahusika, mamlaka, majukumu na utendakazi wa Benki Kuu ya Kenya.