Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 223. Matumizi ya Ziada

(1) Kwa kuzingatia ibara ya (2) hadi (4), serikali ya kitaifa inaweza kutumia fedha ambazo hazijaidhinishwa iwapo–

  • (a) Fedha zilizotengwa kwa madhumuni fulani katika sheria ya matumizi hazikutosha au kumezuka haja ya matumizi ambayo hayakuwa na mgao katika sheria ya matumizi ya fedha; au
  • (b) fedha zimechukuliwa kutoka kwenye Hazina ya Ziada ya fedha.

(2) Idhini ya Bunge ya kutumia fedha chini ya kifungu hiki itahitajika kati ya miezi miwili baada ya fedha kuchukuliwa mara ya kwanza, kulingana na ibara ya (3).

(3) Iwapo Bunge litakuwa limevunjwa wakati wa kipindi kinachotajwa katika ibara ya (2), au vikao vya bunge vinaendelea na bunge kuvunjwa kabla ya idhini kutolewa, idhini lazima itolewe kati ya majuma mawili pindi tu vikao vingine vitakapoanza.

(4) Wakati Baraza la Kitaifa litakapokuwa limeidhinisha matumizi chini ya ibara ya (2), mswada na matumizi ya fedha utawasilishwa kwa mgao wa fedha zilizotumika.

(5) Katika mwaka wowote wa matumizi ya fedha za serikali, serikali ya kitaifa chini ya kifungu hiki haiwezi kutumia zaidi ya asilimia kumi ya fedha zilizotengewa bunge kwa mwaka huo , ila katika hali maalum Bunge limeidhisha kiasi cha juu .