Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 220. Umbo, Yaliyomo na Wakati za Bajeti

(1) Bajeti za serikali ya kitaifa na zile za serikali za kaunti zitajumuisha–

  • (a) makadirio ya mapato na matumizi, zikionyesha tofauti kati ya matumizi ya kawaida na yale ya kimaendeleo;
  • (b) mapendekezo ya kufadhili upungufu wowote unaotarajiwa kwa kipindi cha matumizi;
  • (c) Mapendekezo kuhusu kukopa na madeni yoyote ambayo yataongeza deni la umma katika kipindi cha mwaka utakaofuata.

(2) Sheria za kitaifa zitaonyesha–

  • (a) muundo wa mipango ya maendeleo na bajeti za nchi;
  • (b) wakati mipango na bajeti za serikali za kaunti zitawasilishwa kwa mabunge ya kaunti; na
  • (c) njia na jinsi ya kufanya mashauri kati ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti katika harakati za kutayarisha na mipango na bajeti.