Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 211. Ukopaji wa Serikali ya Kitaifa

(1 ) Bunge kupitia kwa sheria, linaweza–

  • (a) kueleza hali ambazo serikali ya kitaifa inaweza kukopa; na
  • (b) kuweka kanuni za kutoa taarifa.

(2) Kati ya kipindi cha siku saba baada ya Bunge kutoa ombi, Waziri anayehusika na fedha atawasilisha habari kwa kamati husika kuhusu mkopo wowote au dhamana, pamoja na habari yote muhimu ili kuonyesha–

  • (a) kiwango cha madeni yote ikiwa ni pamoja na mtaji na jumla ya faida inayodaiwa;
  • (b) mkopo huo ulivyotumiwa au utakavyotumiwa;
  • (c) Mikakati iliyopo ya kulipa mkopo huo; na
  • (d) hatua zilizochukuliwa katika kulipa mkopo huo.