Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 210. Kutoza Ushuru

(1) Hakuna kodi yoyote au malipo ya leseni yanayoweza kuondolewa au kubadilishwa ila kwa mujibu wa sheria.

(2) Iwapo sheria itaruhusu kufutiliwa mbali kwa ushuru au malipo ya leseni–

  • (a) rekodi ya kufutilia mbali itahifadhiwa kwa umma ambayo itaonyesha sababu za kila kufutilia mbali; na
  • (b) kila kufutiliwa mbali, pamoja na sababu zake lazima zifikishwe kwa Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu.

(3) Hakuna sheria ambayo itamwondolea au kuamrisha mhudumu yeyote wa umma kutolipa kodi kwa sababu za–

  • (a) mamlaka yanayoshikiliwa na afisa huyo; au
  • (b) aina ya kazi anayofanya afisa huyo.