Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 206. Mfuko wa Jumla na Fedha Zingine za Umma

(1) Mfuko wa Jumla umeundwa, ambao utahifadhi fedha zilizozalishwa au kupokelewa kwa minajili ya serikali ya kitaifa, isipokuwa fedha ambazo–

  • (a) kwa sababu maalum zilizotengwa kutoka kwa Hazina hiyo na Sheria ya Bunge na ambazo zitawekwa kwa hazina tofauti ya umma iliyobuniwa kwa lengo maalum; au
  • (b) zinaweza, chini ya Sheria ya Bunge, kuhifadhiwa na taasisi ya serikali iliyozipokea kwa lengo la kugharamia mahitaji ya taasisi hiyo.

(2) Fedha zinaweza kutolewa kutoka kwa Mfuko wa Jumla iwapo tu–

  • (a) matumizi yake yameidhinishwa na Sheria ya Bunge;
  • (b) kwa mujibu wa kifungu cha 222 au 223; au
  • (c) kulipa madeni ya mfuko huo wa jumla kama ilivyoidhinishwa na Katiba hii au Sheria ya Bunge.

(3) Fedha hazitatolewa kwa hazina nyingine yoyote ya fedha za umma ila tu kutoka kwa Mfuko wa Jumla, isipokuwa tu ikiwa kutolewa kwa fedha hizo kumeidhinishwa na Sheria ya Bunge.

(4) Fedha hazitatolewa kwa Mfuko wa Jumla ila tu mpaka Msimamizi wa Bajeti atakapoidhinisha.