Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 200. Sheria ya Kuhusu Sura hii

(1) Bunge litatunga sheria katika masuala yote muhimu au ya lazima kuidhinisha utekelazaji wa Sura hii.

(2) Hasa, sheria inaweza kubuniwa ili iangazie–

  • (a) usimamizi wa mji mkuu, majiji mengine na miji mingine;
  • (b) kuhamishwa kwa majukumu na mamlaka kutoka kwa kiwango kimoja cha Serikali hadi kingine, pamoja na kuhamisha uwezo wa kutunga sheria kutoka kwa Serikali ya kitaifa hadi Serikali za kaunti;
  • (c) taratibu za uchaguzi ama uteuzi wa watu, na kuwatoa mamlakani katika Serikali za kaunti, pamoja na kuhitimu kwa wapiga kura na wagombeaji wa viti.
  • (d) taratibu za mabaraza na kamati kuu pamoja na uenyekiti, mfululizo wa mikutano, uhudhuriaji na upigaji kura; na
  • (e) kusimamishwa kwa muda kwa mabaraza na kamati kuu.