Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 188. Mipaka ya Kaunti

(1) Mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa kwa pendekezo tu–

 • (a) lililopendekezwa na Tume huru iliyobuniwa na bunge kwa lengo hilo; na
 • (b) liliyoidhinishwa na–
  • (i) Baraza la Kitaifa likiungwa mkono na wabunge wasiopungua thuluthi mbili wa bunge hilo; na
  • (ii) seneti ikiungwa mkono na angalau wawakilishi wa kaunti wasiopungua thuluthi mbili ya ujumbe wa kaunti.

(2) Mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa kwa kuzingatia–

 • (a) wingi wa watu na uongezekaji wao;
 • (b) miundomsingi na uhalisia wao;
 • (c) mshikamano wa kihistoria na misingi ya kitamaduni;
 • (d) gharama za usimamizi;
 • (e) maoni ya jamii zilizoathirika;
 • (f) malengo ya ugatuzi wa Serikali; na
 • (g) sifa za kijiografia.