Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 187. Kuhamisha Mamlaka na Majukumu Kati ya Viwango vya Serikali

(1) Mamlaka au majukumu ya Serikali katika kiwango kimoja yaweza kuhamishwa hadi kiwango kingine cha Serikali kwa makubaliano kati ya Serikali hizo mbili kama–

  • (a) mamlaka au jukumu hilo litapata uzito zaidi likitekelezwa na Serikali hiyo itakayolichukua; na
  • (b) kuhamishwa kwa mamlaka au majukumu kunaafikiana na sheria ambazo zinafungamana na utekelezaji wake.

(2) Pale ambapo mamlaka au shughuli imehamishwa kutoka kiwango kimoja cha Serikali hadi kwa Serikali ya kiwango kingine–

  • (a) mipango itafanywa ili kuhakikisha kwamba gharama za utekelezaji wa mamlaka au shughuli hiyo iliyohamishwa imefanikishwa; n
  • (b) uwajibikaji wa kikatiba kwa shughuli au mamlaka utahifadhiwa na serikali iliyopangiwa kulingana na Mpangilio wa Nne.