Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 186. Mamlaka na Majukumu Mahususi ya Serikali za Zaunti na Kitaifa

(1) Isipokuwa kama ilivyotajwa katika Katiba hii, mamlaka na majukumu ya Serikali ya taifa na zile za kaunti, mtawalia,ni kama yalivyoelezwa katika Mpangilio wa Nne.

(2) Jukumu linalopatikana katika zaidi ya ngazi moja ya Serikali ni jukumu lililo katika eneo zaidi ya moja la utawala la ngazi hizo za Serikali.

(3) Jukumu ambalo halijatolewa na Katiba hii au na sheria ya taifa kwa kaunti, ni jukumu ya Serikali ya taifa.

(4) Kuwa yakini zaidi, bunge litatunga sheria ya Jamhuri katika suala lolote.