Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 185. Mamlaka ya Kisheria ya Mabaraza ya Kaunti

(1) Mamlaka ya kutunga sheria ya kaunti yamepatiwa na yatatekelezwa na baraza la kaunti.

(2) Baraza la kaunti, linaweza kutunga sheria zozote muhimu, zinazoshughulikia masuala yanayohusiana na, ufanikishaji wa mamlaka na majukumu yake, na utekelezaji wa mamlaka ya serikali ya kaunti kwa mujibu wa Mpangilio wa nne.

(3) Baraza la kaunti, likizingatia kanuni ya kugawana mamlaka, lina uwezo wa kusimamia kamati ya mamlaka kuu ya kaunti na idara nyingine za mamlaka katika kaunti.

(4) Baraza la kaunti laweza kupokea na kuidhinisha mipango na sera kwa–

  • (a) usimamizi na utumiaji wa rasilmali za kaunti; na
  • (b) kustawisha na kusimamia miundomsingi na idara zao.