Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 2. Ukuu wa Katiba Hii

(1) Katiba hii ni sheria kuu ya Jamhuri na inaunganisha asasi zote za nchi katika viwango vyote viwili vya Serikali na watu wote.

(2) Hakuna mtu anayeweza kudai au kutumia mamlaka ya Taifa ila tu kwa idhini ya Katiba hii.

(3) Uhalali au uthabiti wa Katiba hii hauwezi kupingwa na mahakama yoyote au idara yoyote ya Serikali.

(4) Sheria yoyote, ikiwemo sheria ya mila na tamaduni, ambayo haiambatani na Katiba hii ni batili na kiwango cha ukinzani huo pamoja na kitendo chochote au utendaji unaopingana na Katiba hii si halali.

(5) Sheria za jumla za kimataifa zitakuwa sehemu ya sheria za Kenya.

(6) Mkataba au maagano yoyote ambayo yataidhinishwa na Kenya yatakuwa sehemu ya sheria za Kenya chini ya Katiba hii.