Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

24. Jaji Mkuu

(1) Jaji Mkuu aliye afisini mara tu kabla ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii, ataondoka afisini katika kipindi cha miezi sita tangu tarehe ya kutekelezwa na anaweza kuchagua ama–

  • (a) kustaafu kutoka katika idara ya mahakama; au
  • (b) kwa mujibu wa utaratibu wa kuchunguza chini ya ibara ya 23, kuendelea kuhudumu katika Mahakama ya Rufani.

(2) Jaji Mkuu mpya atateuliwa na Rais, kulingana na Sheria ya Muafaka wa Kitaifa na Maridhiano, na baada ya kushauriana na Waziri Mkuu na kuidhinishwa na Baraza.

(3) Ibara ndogo ya (2) pia itatumika iwapo kuna nafasi za kazi zaidi katika afisi ya Jaji Mkuu kabla ya uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya Katiba hii.