19. Kanuni za Utekelezaji wa Haki za Msingi
Kanuni za utekelezaji wa haki za msingi na uhuru chini ya ibara ya 84 (6) ya Katiba ya awali zitaendelea kutumika.
Kanuni za utekelezaji wa haki za msingi na uhuru chini ya ibara ya 84 (6) ya Katiba ya awali zitaendelea kutumika.
Tume ya Huduma za Mahakama itateuliwa katika siku sitini baada ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii.
adi pale ambapo Mahakama Kuu itaundwa, Mahakama ya Rufani itayashughulikia masuala yaliyopewa Mahakama Kuu.
Kesi zote zilizo katika mahakama yoyote zitaendelea kusikilizwa na uamuzi kutolewa na mahakama husika.
Bunge litatunga sheria mbayo itaweka mikakati na utaratibu wa kuchunguza ustahili wa majaji na mahakimu wote.
Jaji Mkuu mpya atateuliwa na Rais, kulingana na Sheria ya Muafaka wa Kitaifa na Maridhiano.