14. Utekelezaji wa Masharti Yanayohusu Serikali ya Ugatuzi
Tume hizi zitapewa angalau siku thelathini kuchunguza sheria chini ya ibara ndogo ya (1).
Tume hizi zitapewa angalau siku thelathini kuchunguza sheria chini ya ibara ndogo ya (1).
Bunge litatoa mwongozo wa kuhamisha kwa awamu tokea serikali ya kitaifa hadi serikali za kaunti, majukumu yaliyopewa serikali hizo.
Vigezo vya kwanza na vya pili vya misingi ya ugavi wa mapato miongoni mwa kaunti vitafanywa katika kipindi cha baada ya kila miaka mitatu.
Serikali ya kitaifa itafanya marekebisho katika mfumo wa utawala ulio maarufu kwa jina la utawala wa mkoa.
Mabaraza yote ya miji yaliyopo mara tu kabla ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii, yataendelea kuwepo.