Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

9. Uchaguzi na Uchaguzi Mdogo

(1) Uchaguzi wa kwanza wa Rais, Baraza Kuu la Kitaifa, Seneti, mabaraza ya kaunti na magavana wa kaunti chini ya Katiba hii utafanywa wakati mmoja, katika muda wa siku sitini baada ya kuvunjwa kwa Baraza Kuu la Kitaifa kipindi chake kitakapokamilika.

(2) Licha ya ibara ndogo ya (1), iwapo muungano uliobuniwa chini ya Muafaka wa Maridhiano umevunjwa na uchaguzi mkuu kufanywa kabla ya 2012, uchaguzi wa kwanza wa mabaraza ya kaunti na magavana utafanywa mwaka huo wa 2012