Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

8. Umiliki wa Ardhi Uliopo na Makubaliano Kuhusu Maliasili

(1) Katika tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii ardhi yoyote inayomilikiwa na mtu ambaye si raia wa Kenya bila masharti litarejeshwa kwa Jamhuri ya Kenya ili kulihifadhi kwa niaba ya watu wa Kenya, na Serikali itampa mtu huyo kipindi cha miaka tisini na tisa kukodi shamba hilo kwa kulipa kiasi kidogo cha kodi.

(2) Katika tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii, mtu yeyote asiye raia wa Kenya anayemiliki shamba kwa mkataba wa kupangisha uliozidi miaka tisini na tisa, mkataba huo utabadilishwa na kuwa wa miaka tisini na tisa.

(3) Masharti ya Kifungu cha 71 hayataanza kutekelezwa hadi sheria inayorejelewa katika Kifungu hicho itungwe.