Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kiapo ama Kukubali kwa Dhati Mamlaka ya Afisi ya Rais/Kaimu wa Rais

Mimi, ……………… , naapa/nakubali kwa dhati kuwa nitawatumikia watu wote wa Jamhuri ya Kenya kwa bidii katika afisi ya Rais/ Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatekeleza majukumu na wajibu wangu kwa uaminifu katika afisi ya Rais/Kaimu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya; na nitatenda haki kwa wote kulingana na Katiba hii, na kupitia kwa sheria zilizowekwa bila woga, upendeleo, upendo au chuki. (Kama ni kiapo: Ee Mungu nisaidie)